Khadija Mwanamboka Mbunifu wa mavazi na Balozi wa Oxfam Tanzania Aja na Mradi wake mpya aliouzindua hivi kariubuni utakaofahamika kama VVK-GROW-CAMPAIGN PROJECT
Dhumuni la Campaign hii ni kuwainua wanawake wafanyabiashara wadogo wadogo wa chakula lakini pia kufuatilia shughuli zao na kuona ni jinsi gani wanaweza kufaidika na kilimo cha chakula mauzo na kuvumbua changamoto nyingi zinazowakabili katika shughuli zao hizo ambapo itahusish Wasichana wadogo “Grow Girls” ambao watakuwa wanapita katika maofisi mbali mbali na mikusanyiko ya watu wengi ili kuuza bidhaa za wanawake hao wakulima na wafanya biashara wadogo wadogo wa Chakula