Mwanamuziki mkongwe wa nyimbo za asili nchini Saida Karoli, amezikanusha tetesi zilizoanza kuenea tangu jana kuwa amefariki kwenye ajali ya boti katika ziwa Victoria.
Akiongea kwa simu leo asubuhi , Saida ambaye baada ya kutumbuiza kwenye tuzo za Kili wiki iliyopita alielekea Makongorosi Chunya mkoani Mbeya, amesema yupo hai na ni mzima wa afya.
“Mungu wangu, mimi niko hai, ndugu yangu, naomba uwaeleze watanzania kwamba Saida ni mzima, hakuna chochote kilichotokea hata mimi mwenyewe nimeshangaa yaani watu wanapiga simu, ni suala la msiba lakini si kweli,” amesema Saida.