
Baraza la sanaa la Taifa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, leo wamezindua rasmi tuzo za muziki za Tanzania zijulikanazo zaidi kama Kili Music Awards.
Mkurugenzi wa masoko wa TBL kushilla Thomas (katikati) na Kaimu Mkuu Mtendaji wa BASATA Godfrey L. Mngereza wakisaini mkataba mpya wa miaka mitano wa udhamini wa bia ya Kilimanjaro katika tuzo hizoKatika uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam bia ya Kilimanjaro ambayo ndio wadhamini wakuu wa tuzo hizo wamesaini mkataba wa miaka mitano na BASATA wa kuzidhamini ambapo zaidi ya shilingi bilioni 4 zitatumika kuziandaa kwa kipindi hicho.
Tuzo za mwaka huu zitafanyika tarehe 8 June kwenye ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.“Lengo hasa la kusaani mkataba huu ni kuwahakikisha watanzania kuwa tutaendelea kuwapa tuzo hizi na tutaendelea kuzifanya kwa kusikiliza matakwa ya wadau wa sanaa ya muziki Tanzania wanataka nini ili sisi kama wadhamini kuhakikisha wanakipata kile wanachokitaka,
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akizungumza kwenye uzinduzi huo
Kavishe amesema tuzo za Kilimanjaro ni miongoni mwa tuzo kubwa kabisa za muziki barani Afrika.“Wale wanaofuatilia tuzo za muziki Tanzania, barani Afrika na duniani kwa ujumla mtakubaliana na mimi kabisa kwamba tuzo hizi kwa hapa Tanzania na kwa Afrika kwa ujumla ni za ukubwa kuliko tuzo zote zinazotolewa, ilikuwa inatanguliwa na Kora Music, MTV na Channel O awards.
”Nembo rasmi ya tuzo za Kili mwaka 2013
Maafisa wa TBL na BASATA wakizindua nembo ya tuzo za mwaka huuMkurugenzi wa masoko wa TBL kushilla Thomas na Kaimu Mkuu Mtendaji wa BASATA Godfrey L. Mngereza wakizindua nembo ya Kili Music Awards
Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu wa BASATA, Godfrey L. Mngereza alisema juhudi za BASATA na wadhamini wa tuzo hizo, zimeifanya serikali iitambue rasmi tasnia ya muziki kama shughuli rasmi.“Kwahiyo tasnia ya muziki ni rasmi kuanzia January mwaka huu,” alisema Mngereza.“Baraza linachukua fursa hii kuwaasa wasanii kuthamini program hii na kuongeza ubunifu wa kazi zao ili ziwe katika viwango vya kitaifa na kimataifa.”
