
Zaidi ya kilo 200 za madawa ya kulevywa aina ya heroin yamekamatwa na kikosi cha polisi wanamaji katika bahari ya hindi yakisafirishwa kutokea nchini irani pamoja na mabaharia kumi na wawili kutoka nchi ya Irani na Pakistani.
Tukio hilo lililotokea usiku wa tarehe 4 majira ya saa sita usiku waliweza kukamata jahazi hilo na mabaharia kumi na mbili wote wakiwa hawaijui lugha ya Kiswahili wala kingereza na jahazi lao halikuwa na utambulisho wowote wa sheria za majini.
Mkuu wa kitengo cha kudhibiti dawa za kulevywa Godfrey nzowa amesema jahazi Hilo liliweza kukamatwa baada ya kikosa cha polisi cha wanamaji kuendelea na operesheni zake za doria majini na mara baada ya kulitilia shaka waliweza kulikamata na baada ya kulikagua walikamata shehena hiyo ya madawa ya kulevya Aliyoyataja kuwa ni aina ya Heroin ambayo mengi huzalishwa nchini.
