Kwa Waumin Wa Dini Ya Kiislam Wanaamini ya kwamba siku ya Kiama Hata mwanamke mwenye Mimba Ya Mwezi, wiki au hata siku Moja Atajifungua kutokana na Mshtuko wa siku hiyo
Dalili hizi Zimeonekana wazi Huko Ufilipino Baada ya Mshtuko wa Kimbunga kikubwa katika historia ya Ufilipino, Haiyan kiliwafanya wajawazito zaidi ya 75 kupata uchungu kabla ya wakati na kujifungua wakati wenzao wengine wakihangaika kujiokoa na wengine wakipoteza maisha.
Miti iling’olewa , magari yalipinduliwa na majengo yalikatika vipande vipande na kuifanya miji mbalimbali katika nchi hiyo ikitawaliwa na ngurumo za ajabu na kutisha.
Mary Jane Tevez, 16, ni kati ya wanawake waliopatwa na mkasa huo na anasimulia namna alivyoweza kujiokoa kutoka katika nyumba yake iliyoanza kukatika na kuanguka huku akijisahau kuwa alikuwa na ujauzito.
Akiwa na mume wake alikimbia kutoka ndani ya nyumba yake, hata hivyo ukuta wa jirani ulianguka mbele yake hali iliyowafanya washindwe kuendelea na safari na kujikuta wakikwama katika kifusi.
Kilichofuata hapo ni maumivu makali ya nyonga, kwa kuwa ujauzito ulikuwa na miezi saba hakuhisi kuwa unaweza kuwa uchungu, lakini kadri muda ulivyokwenda maumivu yalimzidia na kujikuta akijifungua mtoto kwa kusaidiwa na mumewe.
Mary amempa mtoto wake huyo jina la Yolanda kwa kuwa hilo ni jina la kimbunga kikubwa kilichowahi kuipiga nchi hiyo, “Tumemwita Yolanda kwa sababu ni mkubwa kuliko Haiyan”.