Hili limeshakuwa swala la kawaida sasa kuskia majengo yanaporomoka wakati wa ujenzi ukiendelea katika nchi mbali mbali Duniani, Wakati inatokea hapa kwetu Tanzania tulidhani ni uzembe pekee kwa nchi yetu katika swala la umakini katika kila mmoja wakati wa kutekeleza majukumu yake
lakini kwa sasa inaonekana ni tatizo la nchi nyingi za dunia ya tatu kama Africa, na baadhi ya nchi za Asia
Sasa ni zamu ya Afrika akusini ambapo Mtu mmoja ameripotiwa kufa na wengine 40, wengi wao wakiwa ni mafundi wa ujenzi wanahofiwa kukwama katika kifusi katika eneo la ujenzi la Tongaat, kaskazini mwa Durban.
Watu wapatao 30 wameokolewa, baadhi yao wakiwa katika hali ya taharuki.
Kepteni Zwane amesema watu 11 miongoni mwa waliopelekwa hospitali wamejeruhiwa vibaya.
Hizi ni picha za tukio hilo
Mtu mmoja ameripotiwa kufa na wengine 40, wengi wao wakiwa ni mafundi wa ujenzi wanahofiwa kukwama katika kifusi katika eneo la ujenzi la Tongaat, kaskazini mwa Durban.
Watu wapatao 30 wameokolewa, baadhi yao wakiwa katika hali ya taharuki.
Kepteni Zwane amesema watu 11 miongoni mwa waliopelekwa hospitali wamejeruhiwa vibaya.