Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred
Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred ameumbuka baada ya kuzomewa na wabunge kufuatia kushindwa kuzungumza vyema lunga ya kiswahili, ni jambo la kushangaza hasa kwa mrembo waTanzania ambae amechaguliwa kutoka katika shindano linalohusisha wanyonge kadha anashindwa kuzungumza kiswahili lugha ya Taifa lake
Tukio hilo lilitokea jana wakati wa semina ya wabunge juu ya watu wenye ulemavu wa ngozi ( albino) ilioandaliwa na shirika la maendeleo duniani UNDP ambapo miss Brigitte lilikua linamuhusu kutokana na kuwa balozi wa albino.
Miss Brigitte ambae nanajihusisha na maswala ya kijamii yeye ni balozi wa hisani wa watu wenye ulemavu wa ngozi ambapo amekua akiendesha kampenu mbali mbali ikiwamo kupinga ukatili dhidi ya walemavu hao wa ngozi, lakini uhondo ulikuwa pale mrembo huyo alipotakiwa kuzungumza maneno machache kuhusiana na walemavu hao.
Semina hiyo iliyoongozwa na Mwanyekiti wa kamati ya bunge ya huduma za jamii Magreth Sitta ilihusisha mada mbalimbali ambazo ndizo zilimtia kwenye wakati mgumu miss Brigitte na kukumbwa na kisanga cha kuzomewa.
Wakati tu anaanza kujieleza Brigitte alianza kuzungumza kwa lunga ya kiingereza na taratibu ilianza kusikika miguno kutoka kwa wabunge waliokuwa wapo kwenye semina hiyo.
baada ya kuona hali inaelekea kuwa mbaya miguno imekua mingi mrembo huyo aliomba asome hotuba yake kwa lugha ya kiingereza kwasababu hafahamu vyema kiswahili, ‘waheshmiwa wabunge naomba nitoe speech kwa lugha ya kiingereza kwasababu mimi nimezaliwa kenya na kukulia kenya maisha yangu yote hivo kiswahili changu ni brocken nikiongea hapa mtanicheka” alisema. Kauli hiyo ilizidi kuzua miguno na kufanya hali ya kuto kuskilizana katika ukumbi wa Pius Msekwa Mjini hapo. Hali ilikua mbaya kwa mrembo huyo kwasababu wabunge hao walimtaka na kusisistiza mlibwende huyo azungumze kiswahili ili ujumbe uweze kuwafikia wote walipo mahali hapo kwa ufasaha zaidi.
baada ya kukomaliwa sana na wabunge ili azungumze kiswahili hakuwa na jinsi na kuanza kuzungumza lugha mbayo ilionekana kama ni ki swanglish kutokana na kuchanganya kingereza na kiswahili
story credit : DIMBA
Swali Mbona wakenya wenyewe huzungumza kiswahili? sasa vipi mtanzania huyu ashindwe?