
Pamoja na kujijengea Jina Yeye Mwenyewe Binafsi Alioyewahi Kutwaa Taji La mrembo Wa Tanzania Wema Abraham Sepetu na Mcheza Filamu Maarufu sana Tanzania Lakini pia Ni mtoto wa Kiongozi Ambaye Hakutegemea au Kuegemea Nafasi Ya Baba Ambaye alikuwa ni mtumishi Wa Serekali Ya Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Katika Nafasi za Juu Kabisa Kipindi cha Uongozi Wa Rais Wa Awamu Ya Kwanza Ya Mwl. julius Kambarage Nyerere
Hii Ni HISTORIA FUPI YA MAREHEMU ISAAC ABRAHAMU SEPETU
Balozi Isaac Abraham Sepetu alizaliwa October 15, 1943, ni mzaliwa wa Tabora ila alikulia Zanzibar na alikuwa ni mkaazi wa Zanzibar mpaka mauti yanamfika
Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu alipata elimu yake ya msingi na sekondari katika shule ya St.joseph’s kwa sasa inaitwa Tumekuja huko Zanzibar mnamo mwaka 1952 hadi 1963, vilevile aliweza kujiunga na chuo kikuu huko Berlin nchini Ujerumani mwaka 1964 hadi 1970 alisomea Shahada ya Uchumi,
Marehemu alikuwa anauwezo wa kuongea lugha tatu (3) kwa ufasaha ambazo ni ;- kiswahili, kingereza na kijerumani.
KAZI
Alianza kufanya kazi katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mwaka 1971 hadi 1972 kama Mkuu wa Bizanje Msaidizi na pia alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ikulu. Baada ya hapo mwaka 1972 hadi 1977 alikuwa Naibu Waziri Mambo ya Nje katika serikali ya Muungano Zanzibar, mnamo mwaka 1977 hadi 1979 Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu alikuwa Waziri wa Habari na Utangazaji, Ilipofika mwaka 1979 hadi 1982 alikuwa Waziri wa Utalii na Maliasili .
Marehemu Balozi Sepetu mwaka 1982 hadi 1989 alipewa nafasi ya kuwa Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Moscow na mwaka 1989 hadi 1990 alikuwa Balozi wa nchi ya Zaire, Kinshasa
Katika Serikali ya Mapinduzi
Mwaka 1990 hadi 2000 alikuwa Waziri wa Nchi, Mipango pia alikuwa Mshauri wa Rais, Ushirikiano wa Kimataifa na pia alikuwa Katibu , Kamati ya Pamoja(IPC) CCM/CUF, Zanzibar Mwaka 2001 hadi 2005 alikuwa mbunge wa bunge la Afrika ya Mashariki
Uzoefu wa Kisiasa
Mwaka 1977 hadi 2005 alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi
RATIBA YA MAZISHI
Mwili wa marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu utafikishwa nyumbani kwake eneo la Sinza Mori lililoko jijini Dar es Salaam siku ya kesho Jumanne October 29, 2013 kuanzia saa sita za mchana na mwili huo utaanza kuagwa kwenye mida ya saa nane za mchana na baada ya kuagwa mwili huo utafanyiwa maandalizi ya kusafirishwa kwenda Zanzibar siku ya Jumatano asubuhi tarehe 30, October 2013 na mwili wa marehemu ukifika Zanzibar, Unguja utapelekwa kanisani kwa ajili ya maombi pia utapumzishwa kwenye makazi yake ya daima eneo la Mbozini, Unguja siku ya Jumatano October 30, 2013
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI AMEEN

1 Comment
ndio umejua leo.
salma pole kwa msiba wa mtoto wa dada yako.
naomba kuuliza hivi baba wa wema si muisilam coz nimeona wanaaga