WODI ya Akinamama katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga mkoani tabora inakabiliwa kuingiliwa na wadudu aina ya kunguni ambao wamekuwa kero kwa akinamama wanaokwenda kujifungua.
Wakizungumza kuhusu kunguni hao baadhi ya akinamama katika hospitali hiyo wamesema wanatishia sio tu Afya zao bali hata za watoto wachanga wanaozaliwa na kulazwa katika Wodi hiyo.
Kaimu Bwana Afya wa Wilaya ya Igunga,Paulo Mtumba amekiri kuwepo kwa Kunguni hao katika Wodi ya Akinamama ambayo ni Namba Moja akisema suwala hilo wanalitambua na wamekuwa wakilishughulikia ili kuweza kuepusha wagonjwa na usumbufu wa kunguni hao ambao wanaweza pia kuleta madhara kiafya kwa wanaotumia Wodi hiyo.