
Jana niliandika stori hii kumuhusu rapper mdogo kabisa kutoka Marekani akiwa amekaa jela mwaka sasa baada ya kukamatwa akituhumiwa na makosa ya mauaji na matumizi ya madawa ya kulevya.
Ilisemekana jana Alhamisi 3 angeweza kutoka kwa dhamana,Kwa mara nyingine ikiwa ni mara ya 6, Bobby Shmurda amenyimwa dhamana tena, na Jaji wa mahakama kuu ya Manhattan.
Iliripotiwa Shmurda ambae jina lake halisi ni Ackquille Pollard alitakiwa awe na nafasi nzuri ya kuachiwa kwa kutoa dhamana ya dola milioni na shangazi yake aliweka mali zake ikiwemo real estate yake iliyopo New York.
Mpaka sasa Shmurda amekaa jela siku 351 tokDesemba 2014, Rapper huyo kutoka New York alikamatwa na wenzake wanaounda kundi la GS9 akiwemo Rowdy Rebel na members wengine 13 wote wakapelekwa jela, siku ya kutajwa kesi ya Shmurda tena ni Januari 11 mwaka 2016.
