
Ni wimbo mpya na wa kwanza kumshirikisha mdogo wake Dabo Ambaye amemtambulisha rasmi kama ni mdogo wake anayemfuata Lady Jay Dee alisema alimuacha kwanza ajisimamie mwenyewe na afanye vizuri kabla ya kufanya nae kazi (nadhani ni kuepuka habari ya dada kambeba)
Dabo ni msanii anayefanya muziki wa ragga DanceHall na ameshafanikiwa kwa kupata Tuzo za Kilimanjari Tanzania Music Award zaidi ya mara mbili uzinduzi utafanyinka Nov 28 pale MOG BAR AND RESTAURANT ZAMANI (NYUMBANI LOUNGE)MOROCCO JIJINI DAR ES SALAAM
