Tazama Picha Za Maandamano Ya Wanawake wa nchini kenya walioahidi kuandamana leo hii baada ya mwanamke mmoja kuvuliwa nguo kwa madaya ya kuwa amevaa nusu uchi katikana kituo cha kuegeshea magari cha Uhuru Park
pamoja Na wananchi wa kawaida lakini pia kulikua na viongozi waliojitokeza
Story Iliyoripotiwa na Bbc Ya Juzi na ahadi ya maandamano hayo ambayo hatimae yamefanyika:
Kundi la akina mama wa kilimani waliopo katika mtandao wa facebook nchini Kenya limeapa kufanya maandamano katika bustani ya Uhuru Park tarehe 17 mwezi huu ili kuungana na mwanamke aliyevuliwa nguo hadharani siku ya jumatano kwa kuvaa nusu uchi mbali na kupinga unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake.
Katika kisa hicho kilichofanyika katika kituo cha kuegesha magari cha Embassava jijini nairobi,wanaume wanaodaiwa kuwa makondakta wa matatu walimvua nguo mwanamke huyo na kusema kwamba alikuwa anawasisimua kwa mavazi yake.
Wanawaake hao wameapa kuelekea katika kituo hicho cha magari ya uchukuzi ili kuwaambia makondakta hao kwamba wanawake wana haki ya kuvaa wanavyotaka.
Kanda ya video ya kisa hicho ilichukuliwa na baadhi ya wasafiri na kuwekwa katika mtandao wa jambo net.
Wakenya pia wamepinga tukio hilo kupitia neno MyDressMyChoice katika mtandao wa twitter.
Wanaume wengi wamesema kuwa watajiunga na wake zao pamoja na wana wao wa kike kupinga uhalifu huo siku ya jumatatu.