
Baada ya mkali Jafarai a.k.a Jafarhymes kuonekana kufanya biashara nyingine tofauti na muziki ambao kila mtu ndio kitu alichomjua nacho Jafarai, mara ya kwanza Jafarai alifungua car wash, juzi kati akawa amefungua garage,mashabikiwa wake wakawa wanataka kujua kama mkali huyo amechana na muziki.
Salmamsangi.com ilimvutia waya Jafarai na alithibitisha kuendelea na muziki “Siwezi kuacha muziki kwa sababu muziki ndio uliofanya nimiliki hizi bishara nilizonazo kwa sasa, ila nilikaa kimya nikifuatilia biashara hizi ziweze kusimama” alisema Jafarai “ Kuna ngoma kibao nimefanya zinakuja muda si mrefu kuna moja nimefanya na Ommy Dimpoz na wasanii wengine wakali, nadhani mwishoni wa mwezi Oktoba au mwanzoni mwa Novemba itatoka ngoma na kuendeleza harakati za muziki” aliongeza Jafarai.
