Wakati Lil Wayne alipoachia preview ya “Dusse” mapema mwaka huu watu wengi walishangaa kwa nini alikuwa akimtaja Jay Z.
Hov ni Mungu, Nitakuwa nikimpa sifa muda wote alisema hayo Lil Wayne wakati akipiga stories na MTV, Jay Z alichangia sehemu fulani katika kutengeneza hiyo ngoma alisema.
Lil Wayne huwa aandiki mashairi, anaenda studio anachana kinachokuja kichwani, anasema hakuna ngoma yake anayoandika, kwa hiyo alichokirap usiku ule ndicho kilikuwa kichwani kwake usiku ule.
Lil Wayne amemuongelea Jay Z kutokana na maneno yaliyokuwepo kuhusu wasanii hao , mstari alioimba Lil Wayne akirap kuhusu Jay Z na Kanye West kuhusu Watch The Throne February 2012, Mstari wa Lil Wayne unasema I met a bad red bone, I took the biiii home, I asked her what she want to watch, she said surely no The Throne. Hicho ndicho kilicholeta maneno na kuonekana kama Lil Wayne amewachana washkaji Jay na West.
Inasemekana kwamba Lil Wayne alikuwa amechukizwa na mstari wa kwenye wimbo wa Watch The Throne ambao ulisema, “Im like, Really, half a billi? Nig…really you got baby money, keep it real with guys, guys aint got lady money”, mistari amabyo iliaminika ilielekezwa kwa Baby.
Wayne nae akamjibu kwenye wimbo wa “Im Good”, ngoma kutoka The Carter 4 kuna line anasema “I got your baby money, Kinap your biiii, get that, how much you love your lady money”.
Jay Z nae akajibu kwenye Magna Carta Holy Grails La Familia alichana, “Wanna kidnap wifey, Good luck with that bruh, you must gona hide your whole family, what you think we are wearing black for? Ready for that war, ready for that war ready, you aint ready, yo, you radio”.
Washkaji kama wanakabeef fulani kachinichini hivi, beef business kwenye ngoma tu alafu metaphos tu.
Mmoja akiulizwa pale umemchana fulani anakataa anasema pale na maanisha hivi lakini mwenyewe anajua message sent na aliyechanwa anaelewa nimechanwa, mashabiki wao wanakuwa wanahisi.
Lakini yote kwa yote Lil Wayne anamsalute Jay Hov is God!!