Baada ya kuachana na kurudiana mwishoni mwa mwaka jana, mrembo huyo anayeonekana kwenye video, Lira Galore amethibitisha yeye na Rick Ross wameachana, akipiga stories na Global Grind, Lira alitokwa na machozi pia katika mahojiano hayo.
Alisema “Tuliamua kuachana, na umri wa miaka 22 na hii ilikuwa mara ya kwanza kuwa kwenye mahusiano na niliweka, bado nampenda lakini muda mwingine mambo hayaendi kama unavyotaka yaende, sina muda mrefu toka tuachane, sitafuti wala simuhofii mtu yeyote kwa sasa,kuna vitu vingine vinaendele kwa hiyo tumeachana”
Kuanza mahusiano na rapper mwingine alisema:
“Inatakiwa ujiandae kwa ajili ya aina ya maisha hayo na kila kitu kinachokuja, inatakiwa uwe strong na usijali vitu, lakini ujali wakati huo huo na inakuwa inazidi, sidhani naweza kulimaliza hili”.
Lira pia alisema picha yake akiwa amekaa kwenye mapaja ya Meek Mill, pia tweets za kwamba alitaka aolewe na Wale.
“Sijali kuhusu picha nikiwa na Meek Mill, ilikuwa ni picha tu ya kawaida niliipost kwenye instagram yangu, nilikuwa kazini, nilikuwaga nacheza na ilikuwa ni picha tu, nafhani chumbuko kubwa la kuachana ilikuwa ni watu kuchimbua tweets nilizoandika nikiwa na miaka 17 ambazo nilitweet kuhusu watu tofautitofauti, picha ya Meek, nilmtag picha siku moja na ilikuwa picha hiyo tu ya Meek Mill,. Kila mtu aliendelea kupost picha hiyo na nilihisi kama ningekuwa mwanaume, asingeweza kulivumilia hili, nahisi kipindi kile tulipoachana aligundua alikuwa anachemka, kwa hiyo tulirudiana”