Msichana wa kikenya aliozaliwa katika jiji la Mexico aliyetarajiwa kuchukua tuzo kubwa ya Oscar baada ya kuchukua tuzo kadhaa siku za nyuma kutokana na movie aliyocheza kama mtumwa “12 years a slave” iliyoongozwa na Steve McQueen Ameshinda Tuzo hiyo alfajir ya Jumapili Huko HollyWood
Lupita Nyong’o akipongezwa na Muongozaji wa Filam Aliyoicheza Steve McQueen Pamoja na baadhi ya mastar wenzie waliotokea kwenye Filamu hiyo
Lupita Lupita Lupita lupita ndio anayemake head lines kwa sasa kwenye mitandao yote duniani kutokana mafanikio makubwa aliyoyapata mara baada ya kucheza movie yake hiyo
Lakini inawezekana umaarufu huo unakuja zaidi kutokana na Wapi Alipotokea Lupita Na Rangi yake lakini pia katika umri wake kuwa na mafanikio makubwa kiasi hicho
Ameonekana kuwa mfano kwa wasichana wengi wa kiafrika hata hapa kwetu Tanzania naona kila mmoja amevutiwa na mafanikio hayo hata kuwapa moyo kuwa wanaweza kufikia ndoto zao
Whoopi-Goldberg ni mcheza cinema wa Hollywood aliyeigiza katika filamu ya Sarafina hapa naye akimpongeza Lupita Nyong’o kwa ushindi wa Tuzo ya Oscar
Lupita Nyong’o Ameshinda tuzo hiyo katika kipengele cha Muigizaji bora Msaidizi, kipengele ambacho kimemfanya awe mwanamke wa kwanza kutoka Africa kupata Tuzo hiyo ngumu kupatikana katika kipengele hicho mara nyingi Tuzo hiyo huwa wanapata Main Character
lakini anakuwa mwanamke wa saba Duniani Kuchkua Tuzo Hiyo katika kipengele hicho
History imejiandika na maneno yake yalionukuliwa ni ” ” Na iwe ukumbusho kwangu na kila mtoto kwamba kokote unakotoka, ndoto zako ni halisi.”
katika kipengele cha jana Lupita Anaweza kuwa kamshinda Umaarufu Rihanna Katika Usiku Huo Mmoja