Hii Teknologia sasa jamani imefika mbali kwakweli katika nchi za wenzetu, huko Lima Peru Amerika Ya Kusini Chuo kikuu cha teknolojia cha Peru kimeanza mradi wa kuzalisha maji yatokanayo na njia ya hewa.
Mfumo wa teknolojia hiyo ni kama Bango la matangazo lakini linatengeneza maji kwa njia ya hewa na kuwezesha maji kupatikana ndani yake na hatimae kufanikisha upatikanaji wa maji ya kunywa kwa wapita njia na wananchi kwa ujumla kwa mwenye kuhitaji.
kwa siku mfumo huo una uwezo wa kuzalisha maji lita 100 na tangu kuanzishwa kwa mradi huu january mwaka huu tayari mradi umezalisha maji lita 9450 uwezo huu wa kuzalisha kiasi kikubwa cha maji kwa njia ya hewa unatokana na nchi ya Peru kuishi kwenye unyevu unyevu kwa 83%
Nchi ya peru ni moja kati ya Nchi yenye shida ya maji sana na ndo maana wanateknolojia wameona vi vizuri kutumia ubunifu huo kama njia mbadala ya kuondoa tatizo la maji
Kwa Tanzania pamoja na tatizo la maji ambalo labda halijapatiwa ufumbuzi tunajifunza vipi namna ya kutumia njia mbadala katika kukabiliana na changamoto za matatizo mengi tuliokua nayo kama miundo mbinu ya barabara nk.
TAZAMA NAMNA MFUMO HUO UNAVYOFANYA KAZI KATIKA PICHA HII.