
Mwanamke ambaye ameshutumiwa kumtekeleza mtoto wake katika eneo lililo na watu wengi huko New York katika njia ya chini ya treni, hakuwa fresh toka alipoona boyfriend wake akiuliwa kwa kupigwa risasi yeye akiwa amejificha pembeni, baba wa binti huyo aliiambia ABC News leo.
Binti huyo anayeitwa Frankea Dabbs mwenye umri wa miaka 20, alimuacha mtoto wake huyo mwenye miezi 10 katika eneo lililo na watu wengi huko Manhatan katika kituo cha treni na kurudi na ndani ya treni na kuondoka siku ya JUmatatu.
Binti huyo amekamatwa na kushtakiwa kwa kosa la kumtekeleza mtoto wake na kufanya kitendo hicho kwa mtoto ambae hana umri chini ya miaka 17.
Binti huyo aliwaambia polisi alikuwa hana sehemu ya kuishi kwa hiyo alishindwa kumlea mtoto wake baada ya kuwasli jijini hapo Juni 2.
“Alihisi asingeweza kumtunza mtoto na alidhani alimuacha sehemu salama yenye watu” alisema Stephen Davis msemaji wa NYPD.
Baba yake Aliiambia ABC News leo kwamba hakujua kabisa kama binti yake na mjukuu walikuwa New York, lakini alisema hayupo sawa toka alipoona boyfriend wake akipigwa risasi na kufa.
