Ndio!! Ulivyosoma ndivyo hivyo hivyo ulivyosoma haujakosea…
Mwishoni mwa mwezi Septemba, Gail Simpson mwenye umri wa miaka 63 alikamatwa kwa makosa ya wizi baada ya kuiba Wells-Fargo huko kusini magharibi mwa Miami.
Kwa sasa taarifa zimetapakaa mwizi huyo ni mama wa repa mkongwe mkali Big Pun. Taarifa kupitia Necole Bitchie zimesema kwamba Gail Simpson na Gail Tirado wameunganishwa kama mtu mmoja, wote wanaishi Bronx New York (sehemu ambayo halisi Big Pun anatokea), na sehemu tofauti za Florida. Mwanzo wa kukamatwa alikuwa tayari chini ya uangalizi kwa kujaribu kuiba mwezi Juni, kwa kusema hayo mama wa repa huyo anategemewa kuwa yeye.
Kama hii ni kweli, ni aibu kwamba mama wa repa anayeheshimika kama Big Pun, kuwa mwizi, Kwa juhudi kupata mkwanja ili umsaidie, Simpson aliibia benki mbili mwaka huu kwa ajili ya familia yake na familia kumtuhumu anatumia vibaya estate ya Big Pun.
Pia yamekuwepo malalamiko mwaka 2009 kutoka kwa mke wa Big Pun, Liza Rios kuelekea kwa repa Fat Joe kwa kutengeneza mkwanja kupitia muziki wa Big Pun, mkwanja ambao unamuhusu Liza na familia yake.
Mjane huyo mama yake Big Pun mwezi uliopita alifungua kesi kutokana na TMZ ambapo alisema kwamba hajapata faida yeyote kutoka kwa Big Pun toka mwaka 2005. Fat Joe amejibu kwamba hakuna chochote alichokifanya akapata mkwanja kupitia muziki wa Big Pun toka kifo chake. Pia alisema kwamba anayo makaratasi ambayo yanaushahidi kuhusu hilo.
“Nasikia huruma kwa Liza, lakini nimeshamfanyia mengi kwa ajili yake, Kwa kipindi hiki kigumu kiuchumi sisi kama wazazi tunahitaji kuwa kimya na kufanya kinachostahili kupatia kitu familia zetu” alisema Fat Joe.
Kuna tumaini baada ya kila kitu kikiwa kimewekwa sawa, Familia yote ya Pun inaweza ikaendelea kuwa fresh!! Katika maisha kuna wakati wa kupitia magumu baadae raha…kuna wakati wa kulia na furaha katika maisha!! R.I.P Then Big Pun.