Kimbembe cha kuisaka Ndege Ya Shirika La Ndege la ya malaysia iliyopotea baharini imeingia katika sura mpya baada ya Waganga wa kienyeji wa nchi hiyo kuhusishwa katika swala zima la kutumia uwezo wao na wao katika kuitafuta ndege hiyo
Inasemekana kiongozi mkubwa wa nchi hiyo amemuomba Mganga mashuhuri wa nchini humo bwana Ibrahim mat Zin Almaarufu Raja Bomoh Sedunia Nah Jum VIP’ kufanya lolote ili kuweza kusaidia kufanikisha kupatikana kwa ndege hiyo.
Mganga huyo alifanya Tambiko siku ya jumatatu katika uwanja wa ndege Kuala Lupur ili kusaidia kuipata ndege hiyo number MH370
Wakati Malaysia inatumia waganga kama harakati za kuongeza nguvu katika kuisaka ndege hiyo china yenyewe imeongeza Satellite 10 wote wakiwa katika harakati za kujua ndege ilipo