Huyu ni Mtu mwenye nguvu zaidi Nchini ujerumani kwenye sekta ya soka, Uli Hoeness mwenye umri wa miaka 62 Rais Wa Timu Ya Mpira wa miguu ya Bayern Munich Amehukumiwa kwenda jela miaka 3 na nusu na serekali ya jimbo la Munich baada ya kukwepa kulipa kodi kwa kiasi cha dola za kimarekani 4.85m ambazo ziko katika account yake iliyopo nchini USwiss,
Shauri lilofunguliwa jumatatu lilionyesha anamiliki kiasi cha euro million 15, kumbe uhalisia anamiliki euro million 27.2, Ilipendekezwa kwendajela kwa miaka 10, lakini mahakama ya Munich imemuukumu miaka 3 na nusu, iIa Mwanasheria wake anakataa rufaa kwa mahakama ya juu kupinga adhabu hiyo, baadhi ya mali anazomiliki Rais huyo wa mabingwa wa ulaya ni mwanahisa wa kiwanda maarufu cha sausage cha Nuremberg,