Mwanamuziki mkali wa ngoma ya tubonge, Dr Jose Chamelion imeripotiwa kwamba amelazimishwa kuimba bure na mashabiki kuimba kwenye concert bila malipo yeyote.
Chamelion ambae amekuwa hayupo kwenye show kibao ndogo ndogo za Uganda ambazo alikuwa amepangwa kuzifanya, siku chache zilizopitwa amelazimishwa kuimba mashabiki wa huko Lyantonde na Kalisizo aimbe bure na ilibidi afanye hivyo.
Wazi kabisa Chamelion alilazimishwa kuongeza muda wa kufanya show, ingawa alikuwa kama hataki kukubaliana na wazo hilo , mashabiki walisisitiza na alibaki kwenye steji na kutokana na taarifa zilizopatikana, alipiga show na aliomba msamaha kwa kukosekana kwenye show zilizopita.
Mashabiki walimmiss Jose Chamelion katika show nyingi zilizofanyika akiwa na mizunguko kibao lakini kutokana ni msanii wanaemkubali sana baaada ya kunekana anamaliza show wakagoma wakaona haiwezekani kabisa, jamaa aendelee kupiga show mpaka watakaporidhika, hiyo ni love ambayo wanayo mashabiki wake.