
Davido alishare picha yake na aliandakika miaka mitatu iliyopita hawakuwa na magari…
katika picha hiyo wanaonekana wamezungukwa na magari kama manne hivi ya kifahari, mashabiki wengine walijikuta wakiona ni ngumu kuamini kuwa mtoto wa Omo Baba Olowo na miaka mitatu iliyopita haukuwa na gari wanaona kama anadanganya wakati inafahamika kwamba amezaliwa katika familia ya kitajiri ya mwanasiasa nchini Nigeria..
Lakini inawezekana kweli hakuwa na gari sio wazazi wote hupenda kuwapa watoto wao magari hata kama yapo mengi katika kuhakikisha haharibikiwi.
Katika maoni ya watu sasa baada ya kupost picha hiyo na kuandika “Not luck but blessed…3 years ago we had no cars”
Shabiki wake mmoja anaitwa Dondivajazzy aliandika “why you lie”?
Mwingine anaitwa KRISOKUTWE aliandika “miaka mitatu iliyopita? Andika kitu kingine lakini sio hicho”
Shabiki mwingine anaitwa Chic_ndi_real yeye aliandika Usidanganye Davido miaka mitatu iliyopita haukuwa na gari wakati tunajua wewe ni mtoto wa mwanasiasa na mnamkwanja usitudanganye sisi sio wajinga”. Shabiki mwingine anaitwa Cashinsam aliandika “U lie jooor..you born in golden spoon”..
Hizo ni baadhi tu comments alizoandikiwa Davido baada ya kuandika kwamba miaka mitatu hawakuwa na magari. Nimeona ilikuwa ni mabishano makubwa baada ya post hiyo, mwingine akawashihisha waliocomment kwamba Davido ameandika kwamba hakuwa na magari sio gari……
Angalia hapa jinsi washabiki walivyomshambulia
