Wanaharakati wa wapenzi wa jinsia moja, mawakili na wansiasa wamewasilisha kesi mahakamani nchini Uganda kupinga sheria mpya dhidi ya mapenzi ya jinsia moja nchini humo.
Wanaharakati hao, wanasema kuwa sheria hiyo inakiuka katiba ya Uganda na kuendeleza ubaguzi na kukandamiza uhuru wa kujieleza.
Sheria hiyo ilitiwa saini na Rais Yoweri Museveni mwezi jana na imelaaniwa vikali na jamii ya kimataifa.
Rais wa Marekani Barack Obama ameitaja sheria hiyo kama hatua ya ukandamizaji kwa waganda na nchi kadhaa tayari zimetishia kuinyima Uganda msaada.
Mwandishi wa BBC mjini Kampala anasema kuwa itachukua miezi kadhaa kabla ya kusikilizwa.
Chanzo: BBC SWA