Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa (Mb) akimuelekeza jambo Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo. Mh Philipo Augustino Mulugo kabla ya kuanza kutangaza matokeo ya kidato cha nne mbele ya baadhi ya wanahabari wa vyombo mbalimbali, kwenye makao makuu ya ofisi za wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
Jumla ya watahiniwa waliofaulu kwa Mujibu wa Matokeo hayo ni 23520 kuanzia daraja la I hadi la IV huku katika mchakato huo wasichana waliofaulu katika mchakato huo ni 7178 na wavulana ni 16342.
Aidha Waziri Kawambwa amesema kuwa waliofaulu kwa daraja la kwanza ni 1641, daraja la pili ni 6495 na daraja la tatu ni 15426 na walio feli ni 24903.
Shule bora ni pamoja na St. Francis Girl ya Mbeya, Marian Boys ya Bagamoyo, Feza Boys Dar es Salaam, Marian Girls Bagamoyo na Simini,hizo ndizo zilizopo kwenye tano bora.
huku shule nyingine ni Kanosa, Jude, St. Mary.
KUANGALIA MATOKEO YA MTIHANI WA CSEE na QT, 2012Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT), 2012 yanapatikana katika tovuti zifuatazo
:
www.matokeo.necta.go.tz
www.necta.go.tz
www.udsm.edu.ac.tz
www.moe.go.tz
Matokeo yanaweza kupatikana pia kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwenda namba 15311.
Jinsi ya kutuma ujumbe andika:MATOKEOXNAMBA YA KITUOXNAMBA YA MTAHINIWA(Mfano : matokeoxS0101x0503)