Huwenda jana sakata la umeme kukatika nchi nzima lilikufanya ukose kuona kituko kilichotokea uwanjani wakati ya mechi ya Uruguay na Italy zikichuwana katika mtanange wa kombe la dunia linaloendelea sasa nchini Italy
Baada Ya Kufanya Tukio Kama Hilo Tena Hapo Awali Mchezaji na mshambuliaji wa Uruguay na Liverpool Luiz Suarez hapo mwezi Agosti 2013 alishawahi kumngata Mlinzi wa Chelsea Branislav Ivanovic katika mechi iliyochezwa Anfield, tukio lililomfanya akae benchi kwa mechi 10 na baadae akaomba msamaha.
Kwa haraka miezi 10 baadae amerudia tena wakati wa mechi ya kombe la dunia wakati wa mechi ya Uruguay Juni 24, alionekana akimngata bega beki wa Italia Giorgio Chiellini.
Suarez alionekana akimkimbiza Girogio na mara wote wakaanguka chini huku Suarez akipanua mdomo wake na kumngata Chiellin , Girogio alikuwa akiugulia maumivu huku akivuta tisheti yak echini kumuonyesha refa jeraha alilongatwa na Suarez. Kwa bahati mbaya refa hakuona tukio hilo kwa hiyo hakumpa adhabu Suarez jambo la kushukuru kamera ilipata tukio hilo na watu wengi wanategemea Suarez kupewa adhabu tena.
Ni wiki moja tu baada ya Suarez na meneja wa timu yake kulalamika kwamba amebadilika sana.