NGULI wa muziki wa Dansi Bongo, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ ameanza kuugua tena ambapo tangu Sikukuu ya Iddi hadi sasa yupo hoi kitandani.
Banza alisema Ameanza kusumbuliwa na malaria kali mara baada ya show siku ya sikukuu ya Eid na pamoja na matibabu aliyoyapata hajapata nafuu yeyote mpaka sasa hivyo kuhofia Afya yake
Banza Amesema bado anajiskia vibaya sana na kwamba itambidi kupumzika muziki kwa sasa mpaka Afya yake itakapo tengemaa tena, Lakini pia amewaomba watanzania wamuombee ili arejee katika hali yake ya kawaida
Mpaka Banza anatangaza kuugua na kusimama muziki alikua anafanyia kazi bendi ya Extra Bongo inayomilikiuwa na msanii Ally Choki