Hatimaye yule mbaya wa mwigizaji wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel aitwaye Yvonne Maximilian (22) amenaswa na kuhenyeshwa kortini kisa kikiwa ni kumpiga chupa mwigizaji huyo.
Yvonne aliburuzwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar baada ya kukamatwa maeneo ya nyumbani kwake Kinondoni-Manyanya.
Habari za ndani kutoka kortini zilieleza kuwa awali kesi hiyo ilikuwa isikilizwe na hakimu Agustino Mbando lakini baadaye kulitokea mabadiliko ambapo ilisomwa na Fundi Fimbo.Akiwa mahakamani hapo huku Aunt naye akihudhuria kama mlalamikaji, Yvonne alishuhudiwa akipelekwa puta na polisi.
Hata hivyo, baada ya kesi hiyo kusomwa iliahirishwa hadi Oktoba 17, mwaka huu, itakaposikilizwa tena.Agosti 26, mwaka huu, Yvonne anadaiwa kumjeruhi Aunt kwa chupa tupu ya bia na kumpasua mkono wa kushoto wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bilicanas, Posta jijini Dar.at 9/23/2013