Bilionea wa nchini Australia Clive Palmer ametangaza mipango yake ya kujenga meli pacha ya Titanic lakini hii ikiwa na lifeboats za ziada ili kuwa na usalama zaidi kuliko ya mwanzo.
Zaidi ya karne baada ya Titanic original ambayo ilidhaniwa kuwa haitaweza kuzama baharini lakini ikagonga jiwe la barafu la kuzama kwenye bahari ya Atlantic katika safari yake ya kwanza, Palmer anasema anadhani muda umefika kumalizia safari hiyo ambayo haikumalizika kuelekea New York.
“Titanic ilikuwa ni meli ya ndoto. Titanic II ni meli ambayo ndoto zitakuwa kweli,” alisema Palmer said jijini New York wakati wa uzinduzi wa mradi huo.
Palmer akizungumza katika uzinduzi wa mradi huo
Meli hiyo itakuwa na madaraja yale yale matatu kama meli ya kwanza iliyotengenezwa mwaka 1912, daraja la kwanza, la pili na la tatu na abiria hawatakuwa na uwezo wa kuingiliana kwenye madaraja hayo.
Titanic ya pili itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 2,600 na wafanyakazi 900 na safari itaanzia Southampton hadi New York ifikapo mwaka 2016 katika safari itakayokuwa kama ile ile ya mwanzo na bila shaka bila kuzama tena.
Kwa mujibu wa ripoti ya Mashable, Palmer ameshaanza kupokea ofa za tiketi moja itakayouzwa kwa dola milioni moja.
Story bongo5.com