Baada ya kuwepo kwa uvumi kwamba memba wa Outlawz walichukua majivu ya mwili wa Tupac na kuvuta, mkali huyo ameibuka na kuvunja uvumi huo na kusema hawakufanya hivyo na Tupac yuko hai.
Mapema mwezi huu kulikuwa na uvumi kwamba Tupac anadanganya kuhusu kifo chake , uvumi huo uliibuka tena baada ya ukurasa rasmi wa CIA kutweet kwamba Hapana hawajui alipo Tupac.
Katika mahojiano aliyofanya na Vlad TV repa huyo wa Outlawz E.D.I Mean aliulizwa kuhusu tweet ya CIA na uwezekano wa Tupac kudanganya juu ya kifo chake, alisema hakuna kitu chochote ambacho kitashangaza kuhusu Tupac na alisema usiri utamfanya Tupac aishi milele.
E.D.I Mean anasema Tupac alikuwa smart sana alikuwa akiwaambia wanajua kwamba vitu vya usiri vinauza sana, kwamba siri itakufanya uishi milele, alitoa video inaitwa Thug Life 2013 mwaka jana na kwenye video hiyo alionekana akiwa na ndugu yake ambae ni mrefu kidogo mwembamba ana kipara sehemu moja alionekana akipita kwa nyuma watu wakaanza kusema Yule ni Tupac kwenye ile video.
E.D.I Mean akiwa kama rafiki mkubwa Tupac aliulizwa kuhusu Jermaine Dupri kumfananisha Tupac na Chriss Brown alisema haimuhusu kumfananisha kwani Chriss Brown anafanya fresh kwenye maisha yake ya muziki. Alisema wanategemea watachukia, na labda itawepelekea kufanya ngoma nyingine kama Hit Em Up kwa ajili ya Jermaine Dupri. Alisema Chriss Brown hatakiwi kupitia hata nusu mambo aliyopitia Tupac, Anapenda muziki na anafanya fresh. Alisema E.D.I Mean.