Meriam Ibrahim yule mwanamke wa Kisudani aliyenusurika kifo baada ya kuhukumiwa kunyongwa kwa kosa la kuiasi dini yake ya kiislam nchini sudan ameachiwa huru na sasa ameshaondoka Nchini Sudan baada ya kuhifadhiwa eneo ambalo lilikuwa ni siri kwa usalama wake
U.S State Department Ilisema wakati wa taarifa yake mjini washington DC ya kuwa Meriam sasa yupo huru na salama na mwenye ulinzi japo ripoti hiyo haikuweka wazi kuwa Meriam ameondoka Sudan kwenda Marekani sehemu ambayo ilitegemewa meriam na familia yake kuhifadhiwa kama wakimbizi wa kisiasa
Taarifa Kutoka Suda zimesema hazikumkamata Meriam isipokuwa alitakiwa kuonyesha makaratasi ya kusafiria na hiyo iligundulika uwanja wa ndege tangu alipokuwa ameachiwa huru alipokuwa ana board kuondoka Sudan leo… Anapoelekea bado hapajajulikana