
Happiness Watimanywa, msichana pekee kutoka Tanzania aliyeweka historia ya kuongoza nchi zaidi ya 150 za mtandao wa IGCSE katika somo la Uhasibu kwenye mitihani ya kidato cha nne mwaka 2010.
Happy (19) ni mzaliwa wa familia ya kawaida sana ya Mr Louis Roussos ya Morogoro.
Wadogo zake Angel na Romeo sasa wanasoma St. Constantine shule iliyomtoa Happy. Pia, Happiness Watimanywa amewahi kusoma Laureatte International School ya Dar-es-salaam, ambapo akiwa hapo, alikutana na mwalimu wa michezo Mr Tchalewa Ndeki ambaye alimfungulia mipaka mingi Happy
Akiwa Laureatte, Happy aliwahi kwenda China na South Korea akiwa na wanafunzi wenzake katika matamasha mbali mbali ya elimu na michezo.
Baada ya kumaliza kidato cha nne, Happy alifanikiwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Strathclyde cha UK ambapo anasomea digrii ya Biashara.
aliamua kujihusisha na masuala ya urembo wakati akiwa likizo na kufanikiwa kutwaa Taji la Miss Dodoma, na Miss Kanda ya Kati na hatimaye kuingia kwenye kambi ya Miss Tanzania.
Akiwa Miss Tanzania, Happy alikuwa ni mshiriki wa kwanza kuingia Nusu Fainali ya mashindano hayo kwa kutwaa taji la Redds Miss Photogenic 2013.
