Mgomo mkubwa zaidi wa wafanyakazi wa machimbo ya madini ya Platinum nchini Afrika Kusini kulalamikia mishahara duni…
Chama cha wafanyakazi wa sekta ya madini nchini humo AMCU kimesema kuwa zaidi ya wafanyakazi elfu sabini wameingia katika mgomo huo kwanzia siku ya jana ya Alhamis hadi matakwa yao yatakapotimizwa.
Huu ni mgomo mkubwa zaidi kuwahi kutokea katika secta ya uchimbaji wa madini ya Platinum tangu mkasa wa mwaka juzi wa Marikana ambapo wachimba migodi wapatao 34 walipigwa risasi na polisi walipokuwa wakiandamana kuendeleza mgomo wao uliotajwa na serikali kuwa haramu.