
Mtu mmoja huko Thailand amehukumiwa kwenda jela miaka 37 baada kumtukana mbwa wa Mfalme,wakili wake amesema. Thanakorn Siripaiboon, (27) ametuhumiwa kwa kosa la kufanya udaku kwenye post yake kwenye face book kuhusu mfalme na mbwa wake,mwanasheria Pawinee Chumsri aliiambia AFP “Kulikuwa na post kwenye face book yake Desemba 6 ambayo ilimdhihaki mbwa wa mfalme” alisema.
Thailand ni moja ya nchi duniani zenye sheria kali za kifalme, mtu yeyote akikutwa na kosa la kumtukana mheshimiwa lakini pia mfalme Bhumibol Adulyadej, au malkia,mrithi wake anafungwa miaka 15 jela kwa kila kosa.
Thanakorn fundi wa magari, atafungwa miaka 37 jela,Bhumibol ambaye ni mfalme aliyetawala muda mrefu,inawaunganisha katika taifa lililogawanyika sana na uchumi wake, mambo ya kijamii yameendelea kupewa nafasi sana nchini Thailand.
Kwa miaka 10 iliyopita mbwa wake kipenzi, ambaye anaitwa Tongdaeng ambae alipotea ambaye anasifiwa kwa uaminifu wake na heshima, amukuwa akitumiwa kama mfano jinsi Wathailand wanatakiwa kuwa.
