
Kama unakumbuka siku ambayo Tupac alishutiwa alikuwa akitoka kuangalia pambano la ngumi Las Vegas likiwa ni pambano lililomhusisha rafiki yake mkubwa Mike Tyson.
“Mike Tyson amefunguka kuhusu kitu kikubwa anchokumbuka kuhus Tupac katika urafiki wao, Alifunguka kupitia AMA Ask Me Anything na Reddit “Alikuwa mshikaji mmoja fresh sana, rafiki yangu wa karibu, kumbukumbu yangu kuhusu Tupac ni pale siku moja alipoingia club na alirusha kinoma siku hiyo, alikuwa na miaka 19 tu” Alisema Tyson.
Tupac alipigwa risasi huko Las Vegas Nevada akiwa ameka kwenye siti ya abiria akiwa anaendeshwa na alifariki Septemba 13 1996 akiwa na umri wa miaka 25.
Tyson na Tupac walihusika kwenye makala ya ESPN inayoitwa One Night In Vegas ikionyesha urafiki mkubwa kati ya aliyekuwa bingwa wa ndondi duniani na rapper mkali Tupac na tukio la Tupac usiku ule aliopigwa risasi Tupac.
Juzi kati National Geographical Channel walionyesha makala ya Tupac kuanzia Julai 6 hadi Julai 8, Suge Knight mmiliki wa zamani wa Death Row Records alituhumu akisema Polisi wanajua alipo Tuapc kwa sababu mpaka sasa hivi hakuna mtu yeyote alikamatwa kutokana na kifoo hicho na kesi bado iko dilemma Central Intelligence Agency CIA walitwet walisema “No. We don’t know where Tupac is #twitterversary,” Hiyo ndo ilikuwa tweet ya CIA.
Siku ambayo Tupac alikufa ni kama alitabari kifo chake alikuwa amelewa sana na hakutaka mtu yeyote aungane nae
