
Uchaguzu wa kenya umechukua sura mpya sasa baada ya Tume ya Uchaguzi na mipaka nchini Kenya IEBC kuamua hesabu zifanyike kwa mkono yaani ( Manual) badala na mfumo wa kidigitali ambao ulianza kutumika hapo awali, mpaka sasa imebidi kura kutoka majimbo yote zisafirishwe kwenda Boma mahali ambapo kura hizi zitahesabiwa kwa jumla.
Hata hivo baadhi ya wananchi wa wakenya wameanza kutilia wasiwasi zoezi hilo la uhesabuji wa kura linavoendelea mpaka sasa
Uchaguzi wa kenya ulifanyika juma tatu tarehe 4 ambapo wakenya walipata nafasi ya kumchagua kiongozi wanaotaka awaongoze.
Tume ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya IEBC imetangaza kutolewa matokeo ya uraisi siku ya ijumaa au Jumatatu ya wiki ijayo.
