Kundi la muziki wa kizazi kipya la P.STAR linaloongozwa na goli kipa wa zamani wa timu ya Yanga ambaye pia ni kocha wa makipa katika timu hiyo Bw. Juma Pondamali (Mensah), akiwa na kundi hilo, wamerekodi wimbo maalum wa timu ya Yanga, unaoitwa “Yanga Mbele” ukiwa ni wimbo wa kushangilia na kutoa hamasa kwa Wanayanga wote.
Lengo la kurekodi wimbo huo wa “Yanga Mbele” ni kutaka wanachama wa timu ya Yanga kuweza kununua CD, ambapo baadhi ya pesa zatakwenda kwa timu hiyo kwa ajili ya kuchangia pesa katika kujenga uwanja wa timu hiyo.
“Kampeni ya kuipigania timu yetu ya Yanga, tumeipa jina la YANGA NI MIMI, kama wewe ni mwanachama wa Yanga amini kwamba Yanga ni wewe, na wewe ndiye unayeweza kuleta mabadiliko makubwa ndani ya Yanga, ili mabadiliko yeyote yatokee ni lazima wewe uamue kufanya mabadiliko” Haya ni maneno ya Pondamali Mensah.
Yanga inao wanachama kwa maelfu nchi nzima, kwa hiyo wanachama ambao wanamapenzi mema na wanaipenda Yanga na wangependa waone timu yao inapata maendeleo ikiwemo ni pamoja na kujenga uwanja, basi hii ni njia moja wapo ya kuanza safari hiyo ya kuelekea kupata maendeleo kwa timu yetu.
Mabadiliko ndani ya Yanga hakuna mwingine anayeweza kuyaleta, kama sisi wanachama tusipoamua kwa moyo wa dhati kuichangia timu yetu, kwa kuanza kuununua wimbo wa “Yanga Mbele” utaweza kabisa kuichangia timu ya Yanga, kama kila mwanachama akinunua wimbo huu kuna uwezo wa kupata pesa nyingi ambapo tutaweza kufungua na kuanzisha njia ya tamanio lililo la wengi.
“Wanayanga tujifunge mkanda kwa hili kila mtu ajitahidi kupata wimbo huu, usikubali mtu akurushie kama wewe ni Mwanayanga, wimbo utatoka rasmi tarehe 20/3/2016 siku ya Jumamosi” anaongeza Mensah.
Zimeshawahi kutoka nyimbo kadhaa za Yanga lakini ni muda mrefu umepita hakuna wimbo mpya unaowapa burudani Wanayanga wanapokuwa viwanjani katika kuchochea ushabiki na shangwe uwanjani, hivyo tunaomba Wanayanga kujitoa kuisaidia timu yao kuleta maendeleo, na kuweza kujenga uwanja wake na huu utakuwa ni mwanzo mzuri ulioanzishwa na Pondamali na kundi lake la P.Star.
“Mimi Ni Yanga”
Related Posts
-
-
Unaweza Ukaenda Kwenye Fasheni Show Nyingine Ukaishia Kukimbia! LOL
-
Kanye West Atoa Darasa La Fasheni Ikiwa Ni Mradi Wa Kuhudumia Jamii
-
Vevo, Wametweet Maneno Yalioonekana Kumdhalilisha Kim Kardashian Na Mwanaye North, Wahabiki wawacharukia
-
Mgomo Mwingine Mkubwa Kuwahi Kutokea Migodi Ya Madini Ya Platinum Nchini Afrika Kusini
-
Kauli ya Ney Wa Mitego Kuhusiana na sakata la Ommy Dimpoz
-
Daraja La Mto Mzinga Latengemaa Baada Ya Kusombwa Na Mafuriko