Ice Cube repa ambae alifanya vizuri sana katika siku za nyuma na kujizolea heshima kubwa na umaarufu mkubwa kwa ngoma zake kali kama “Bow Down” na nyingine amejitokeza na kusema bila mkali James Brown kusingekuwepo muziki wa rap.
Ngoma nyingi za Ice Cube zilikuwa na sample na marehemu muimbaji wa soul James Brown, katika mkesha wa Get On Up, mkongwe huyo alisema James Brown alitoa mchango mkubwa sana katika kuindeleza rap.
“Tusingekuwa na Rap music bila James Brown” alisema Ice Cube kwenye video iliyopostiwa na Hip Hop Dx.
Zaidi ya hapo Ice Cube alisema kwamba Brown alikuwa na ushawishi zaidi sio tu kwa muziki.
“Kila mtu ambae alijaribu kuwa funky aliiba kutoka kwa James Brown, ambapo tulianza kufanya miaka ya 1980, alifanya hivyo miaka 30, 40, 50 iliyopita.
James Brown alikuwa muimbaji maarufu aliyejulikana kama “The Godfather od Soul” na ngoma zake zikuwa sampled katika nyimbo kibao za rap, ikiwemo za Nas, EPMD na Dr. Dre.
Kwenye filamu ya “Get On Up” yupo Chadwick Boseman, ambae ameigiza kama Jackie Robinson kama Brown, The Roots Black Thought, Aloe Blacc na Jill Scott pia wamo katika filamu hiyo.
“Tusingekuwa Na Muziki Wa Rap Bila James Brown” Afunguka Ice Cube
Previous Story
Drake Asema Yeye Na J.Cole Ndo Wafalme Wa Rap Kwa Sasa
Related Posts
-
-
Fainali Kagame Cup Ni Azam FC Na KCCA
-
Picha:Peter Okeye Wa P’square Afunga Ndoa Ya Kimila,Msanii Wa Tanzania Diamond Ni Moja Ya Waalikwa
-
Chris Brown Huenda Akarudi Tena Jela Kwa Kosa La Kuwatolea Maneno Machafu Washabiki wake
-
Video: Tubonge Ya Dr.Jose Chameleone
-
Mabaki Ya Ndege Iliyopotea Ikiwa Na Wachezaji Miaka 54 Iliyopita Yaonekana Huko Chile
-
Kesi Iliyokuwa Ikimkabili Justin Bieber Ya Kumshambulia Dereva Wa Limo Yafutwa