
Mkali wa Dancehall Diva Cindy Sanyu inasemekana amepost comment kumuhusu Leah Kalanguka ili kupata attention kwa ajili ya video ya wimbo wake mpya unaoitwa Zalawo. Hii inaonekana kama stunt tu trick katika biashara ya muziki. Cindy alimchana miss Uganda huyo katika ukurasa wake wa face book.
Aliandika “Miss Uganda is really ugly, now you know the truth”
Kama unavyoweza kuifikiria comment mbaya kama hii alafu ngoma yake inakuja huyu anatafuta kick, na haikushangaza kwa sababu stori hiyo imekamata Afrika Mashariki yote, kama amefanikiwa. Lakini haraka Cindy alikana kufanya hivyo na kusema account yake ya face book imeingiliwa (hacked).
Kabla ya yote haya, Diva huyo Cindy alikuwa amepanga kuachia video ya wimbo wake mpya “Zalawo” wiki hii, kwa hiyo Cindy alitengeneza kitu fulani ambacho kilimfanya awe midomoni mwa watu.
