Pichani ni Wananchi wakiwa katika hali ya taharuki baada ya moto kuzuka katika Jengo la iliyokuwa tawi la Benki ya NBC Kichwele jirani na makao makuu ya Ofisi za MeTL jioni hii.
Hata hivyo chanzo cha moto huo bado hakijajulikana mpaka sasa.
Na jitihada za kuuzima moto huo zinaendelea kutoka kwa kikosi cha zimamoto wakisaidiwa na Polisi.
Baadhi ya Wananchi wakishangaa moshi mzito uliokuwa ukifuka kutoka ndani ya jengo hilo Ground Floor inayotumika kama Ghala la kuhifadhia mizigo.
Mmoja wa wakazi anayeishi gorofa za juu za jengo hilo akifannya mawasiliano na ndugu zake.
Askari wa Kikosi cha zimamoto katika jitihada za kuuzima moto huo ambao chanzo chake hakijajulikana.
Muonekano wa Gorofa hilo kwa juu linaloungua moto katika gorofa ya chini inayotumika kama ghala la kuhifadhia mizigo.