Inadaiwa Mjukuu wa Hayyati Nelson Mandela Mandla ambaye ni mjukuu wa kwanza wa mzee Madiba Mandela , alimshambulia mwalimu, Mlamli Ngudle na hata kumtisha kwa bunduki baada ya Mwalimu huyo kuligonga gari la mmoja wa marafiki zake mwaka jana, kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari tarehe 24 baada ya kusikilizwa kwa muda katika mahakama ya Mthatha..,
Mandla alirithi wadhifa wa babu yake kama kiongozi wa kitamaduni.
Mwendesha mkuu wa mashitaka aliwasilisha mahakamani mashitaka mawili dhidi ya Mandla,la kwanza likiwa kumshambulia mtu na pili kumtisha kwa silaha..
bado hajasema ikiwa anakiri au kukanusha mashitaka hayo lakini wakili wake aliitaka mahakama kuahirisha kesi dhidi yake akisema kuwa alipokea mashitaka hayo leo tu na kuwa anahitaji muda zaidi kuyatathmini.
Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya vyombo vya habari nchini Afrika Kusini.
Pamoja ana cheo alichonacho Mandla amekuwa ni mtoto mtukutu na mwenye kuleta vioja kila kukicha kwenye familia hiyo maaruu zaidi Africa Na Duniani