
Mlinzi wa repa wa G. Unit, 50 cent ameripotiwa amempiga ngumi kijana mwenye umri wa miaka 16 baada ya kujaribu kupiga picha na video msanii wa hip hop 50 cent akiwa na mtoto wake.
Vyombo vya dola vimesema 50 cent alikuwa akifanya manunuzi Burbank Town Centre akiwa na mtoto wake wikiendi iliyoisha, Lazzeri Frazier akiwa na mtoto wake mwenye umri wa miaka 16 alimuona 50 cent na kuanza kuchukua video kwa kutumia simu yake.
Mlinzi huyo wa 50 cent alichukua simu hiyo ndipo walipoanza kupigana, taarifa zinasema mtoto wa Frazier alijaribu kuamua ugomvi huo ndipo alipopigwa ngumi kwenye uso na mlinzi huyo.
50 cent amabe ahusiki kwenye kesi, imeripotiwa hakuongea na polisi kuhusiana na tukio hilo, Mlinzi huyo aliondooka kama polisi wajafika kwenye sehemu hiyo. Mashahidi waliulizwa walikubali na kuelezea tukio lote.
