
Mtoto Moureen Julius(12), amejinyakulia kitita cha shilingi Milioni tano katika fainali za Shindano la “MO KIDS GOT TALENT 2013” lililofanyika kwenye hoteli ya Ledger Plaza Bahari beach lililoanza tarehe 25 hadi tarehe 28 mwezi huu ambapo fainali zilifanyika.
Shindano hilo lilijumuisha watoto zaidi ya mia mbili ambapo kila mmoja alijipatia nafasi ya kuonesha kipaji chake vikiwemo kuogelea, kuimba, kucheza, karate na vingine vingi.
Watoto 15 walichuana katika nusu fainali na kuchujwa hadi kufikia watoto watano na mwisho wa siku kupatikana SUPA STAA Moureen Julius aliyewafunika wenzake kwa kipaji alichonacho.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutangazwa mshindi wa kwanza aliyejinyakulia kitita cha sh.millioni tano, Mtoto Moureen Julius alisema pesa hizo alizoshinda atazitumia kwa kulipia ada na vifaa vingine vya shule.
Shindano hili la “MO KIDS GOT TALENT 2013″ liliandaliwa na Frost Africa na kudhaminiwa na Mohammed Enterprises Tanzania Ltd. (MeTL) Group.
PICHA
Pichani juu na chini washiriki wa shindano la “MO Kids Got Talent 2013″ wakiendelea kuonyesha vipaji vyao wakati wa fainali za shindano hilo.
Jaji Hidaya Njaidi akitoa maoni yake kwa washiriki (hawapo pichani) waliokuwa wakichuana kuwani Shilingi Milioni 5 za Kitanzania zilizotolewa zawadi na Kampuni ya MeTL Group.
Jaji Mkuu wa shindano la “MO Kids Got Talent 2013″ Salma Mziray akitoa maoni yake kwa washiriki waliofanikiwa kuingia tano bora.
Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Bi. Fatema Jaffer na Afisa Mtendaji Mkuu wa Frost Africa, Bw. Peter Sekasiko wakionekana kufurahishwa na vipaji vya watoto hao.
Jaji Kiongozi wa shindano la “MO Kids Got Talent 2013″ Salma Mziray akitoa shukrani kwa kampuni ya MeTL kwa kuweza kuibua vipaji vya watoto na vijana.
Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Bi. Fatema Jaffer, akikabidhi kitita cha Shilingi Milioni tano za Kitanzania kwa Supa Staa wa Shindano la “MO Kids Got Talent 2013″ Moureen Julius (12). Wanaoshuhudia tukio hilo ni baba mzazi wa Moureen pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Frost Africa, Bw. Peter Sekasiko ambao ndio waandaji wa shindano hilo.
Sehemu ya watoto, wazazi/walezi waliohudhuria fainali za shindano la “MO Kids Got Talent 2013″ lililofanyika mwishoni mwa juma kwenye hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach.
