Elena Komleva Mwanamke Kutoka Asili ya Cheliabinsk Kusini mwa Russia, Ametoa kali baada ya kufanya tangazo na kuliweka kwenye mitandao ya kijamii akitangaza kutafuta mwanaume atakayeweza kumpa mimba ili kuachana na shida za mama yake mzazi kumsumbua kuhusu kupata mtoto akisisitiza kuwa mama yake atakuwa tayari kuchagua mwanaume huyo kikubwa anachotaka ni mjukuu
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 29 ambaye ni mtaalam wa mambo ya urembo wa kucha alitoa tangazo hilo na kusema huyo mama yake atahusika kuchagua mwanamme atakae shinda
Aliandika hivi
“Mama yangu anahitaji mjukuu atakayempa nguo zote za kitoto alizozikusanya kwa muda mrefu , lakini hakuna anayetaka kunioa mpaka sasa, sasa kama wewe ni kijana mkakamavu na mwenye afya nzuri tuwasiliane”
Na mwisho wa yote mama yake atahusika kuchagua washiriki wa tukio la kumpa mimba binti huyo na mama mtu atapata nafasi ya kumtangaza atakayeshinda, Watakao jitokeza watafanyiwa usaili muda si mrefu kwa kipindi hiki anachojiandaa na kuwapanga washindani wa mchuano akishirikiana na mama yake
Kuna wakati mama zetu imani ya kimungu inawatoka pale wanapoamini swala la kuzaa ni uwezo wa binadamu kwasababu wao walizaa