
Kampuni inayoongoza kwa kutoa huduma ya mawasiliano ikiwa na wateja milioni 300 katika nchi 20 za Afrika na Asia imetangaza kuwa mshindi wa shindano la Airtel Trace Star atatangazwa mwezi huu wa Januari tarehe 10 2015 taarifa kutoka Kenya zimeeleza.
Wakati wa kipindi shindano likiendelea , majaji Chris Adwar, Atemi Oyungu na Wyre walichuja watu hadi kufikia watu sita wa mwisho, ambao walipatikana kwa kupiga namba 0900 733 733 kati ya mwezi Oktoba 5 2014 hadi Desemba 1, 2014.
Hao sita waliochaguliwa walitazamwa ubora wa uwezo wao, uhalisia, tone na range.
Shindano pia lilihusisha mashabiki kuchagua kwa kuwapigia kura washiriki ambao wao walikuwa wakiwapenda kupitia namba 33733 aliyepata kura nyingi pia aliingia kwenye sita bora.
Washiriki hao sita waliobaki katika fainali ni Bliss, Webi, Joy, Njeri, Phyllis na Trina ambapo wananchi wamepewa nafasi ya kupigia kura mshiriki wanaompenda aweze kuwa star mkubwa Afrika. Mshindi kutoka Kenya pia atakua sehemu ya shindano la Pan African Airtel Trace Music Star shindano ambalo linahusisha nchi 13 itakuwa mwishoni mwa mwezi wa Februari 2015.
Mshindi wa Airtel TRACE Music Star ataondoka na kitita cha kiasi cha milioni 1.5 na tiketi ya kushiriki shindano la Pan African.
Mshindi wa kwanza ataondoka na simu ya thamani ya 90,000 ya Kikenya na shilingi laki moja ya Kikenya. Na mshindi wa pili ataondoka na simu ya thamani ya laki 50,000 na pesa taslimu 50,000.
Mshindi wa Pan African atachukua kitita cha euro 30,000 pesa taslimu, deal ya kurekodi Universal Music, akisimamiwa na AKON na safari zenye kiwango cha nyota 5.
