Wasanii wawili ambao wanafanya fresh katika muziki wa Uganda, waite Radio na Weasel wamenusurika kufa baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Entebe wakati wa mchana wakiwa na muimbaji na mtayarishaji wa mapigo ya muziki Washington ambae walisafiri nae.
DMC Subaru ambayo ilikuwa ikiendeshwa na meneja wao Chagga wakitokea Entebe Airport gari ilipata matatizo na kuwaka moto na kusababisha kuiacha gari hiyo.
Gari hiyo ilizengua ikiwa ni mida ya saa 8 mchana karibu na Lubaga Cathedral, na kusababisha msongamano wa magari na kuwa tishio kwa watumiaji wa barabara.
Mzozo huu ulitokea siku ya Jumatano siku ambayo ilikuwa ndo mkesha ya mkesha wa mwaka mpya wa 2015, ilibaki kidogo tu mwaka huu wa 2015 tuwaongelee vingine Radio na Weasel.
Radio na Washington walisaidiwa na meneja wa David Lutalo, ndio aliowasaidia huku wasafiri wengine wakiwacheka huku mashabiki wao wa ukweli wakiwasifu kwa kuepeka kifo.