Binti mmoja mwenye umri wa miaka 21 kutoka jimbo la Florida Marekani ametumia zaidi ya Tshillingi 33,000,000 ili kufanya upasuaji wa kuwekewa titi la tatu ili asipendwe na wanaume.
Msichana huyo Jasmine Tridevil alisema hakutaka tena kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume yeyote na alichoka kutongozwa kila wakati ndio maana akaamua kufanyiwa upasuaji huo na kuwekewa titi hilo katikati ya matiti yake mawili ili asiwe na mvuto.
Msichana huyo ambaye ana malengo ya kuanzisha kipindi katika televisheni ya MTV alisema alimtaarifu mama yake kuhusu uamuzi wake huo ingawa mzazi huyo hakuonekana kufurahia.