Tulimpenda lakini, Mungu amempenda zaidi, Baada ya kukaa hospitali toka Januari 31 mwaka huu, hatimaye Bobbi Kristina, amefariki dunia Jumapili Julai 26 akiwa na umri wa miaka 22.
Mtoto huyo pekee wa kike wa marehemu Whitney Houston na Bobby Brown alikaa hospitali kwa miezi 6 huko Georgia baada kukutwa ameanguka bafuni akiwa hajijui uso ukiwa umezama kwenye maji nda ni ya bathtub nyumbani kwake ilikuwa Januari 31.
Baada kupatiwa matibabu alihamishiwa hospice care mwezi uliopita na Jumapili ya jana amefariki.
“Hatimaye amepumzika kwa amani akiwa kwenye mikono ya Mungu” tunataka tena kumshukuru kila mmoja kwa upendo wao usioelezeka na support kwa miezi michache iliyopita” Familia ya Houston iliiambia Us Weekly katika maelezo yao
Mama yake Whitney Houston alifariki miaka mitatu iliyopita Februari 2012 akiwa na umri wa miaka 48, baada ya kifo chake jana Mastaa wengi wametoa salamu zao za rambirambi baada ya taarifa kuenea katika mitandao jana jioni .
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, bu she gone too soo. Endelea kutembelea www.salmamsangi.com kwa kinachoendelea……