
Mtoto mwenye miaka 8 ameuawa kwa kupigwa risasi baada ya kupita dirishani ikitokea nje na kumpata kifuani akiwa amelala.
Askari wa Detroit wanasema risasi hiyo iliyomuua Jakari Pearson, inaweza ikawa ni matokeo ya ugomvi wa nyumbani uliotokea majira ya saa 1:15 usiku Jumatano ambapo mtu asiyejulikana alitembea nyumba na kuanza kufyatua risasi kwenye nyumba hiyo.
Jakari alikimbizwa hospitali baada ya kupigwa risasi lakini baadae ilitangazwa amefariki dunia alipowasili hospitali. Mama yake pia alipigwa risasi na jinsi anavyoendelea kwa sasa bado haijajulikna.
Mashuhuda wanasema kufyatuliwa risasi kulifuati baada hali fulani ya kutoelewana kwa mama wa mtoto huyo na mtu huyo. Mpaka sasa hivi Polisi hawatoi tarifa nyingi. Sgt Michael Wood hawatatoa taarifa zaidi kuhusiana na mauaji hayo lakini alisema wachunguzi bado wanafuatilia muuaji huyo.
“Tuna wazo zuri nani tunamtafuta, kwa bahati mbaya hatuwezi kuongea sana kuhusu swala hili sana kwa sababu ni mapema sana bado tuko kwenye uchunguzi, tunatumaini jamii inaendelea kuongea na sisi na kutupa taarifa kwa hiyo tunaweza kumtafuta mtu huyo na kumpeleka mbele ya sheria.
