Mtu mmoja mkazi wa Kawe Mzimuni jijini Dar es Salaam ameuawa katika chumba kimoja walichokuwa wakiishi wasichana wawili huku uchunguzi waawali ukubaini kuwa mtu huyo alichomwa na kitu chenye ncha kali na kusababisha kuvuja damu nyingi na kupoteza maisha.
kutokana na tukio hilo, umati mkubwa wa watu kutoka maeneo mbalimbali ya Kawe Mzimuni walionekana katika eneo la tukio wakishangaa mauaji ya mtu huyo anayedaiwa kuwa alikuwa ni mjasiriliamali ambaye alikuwa akiishi sehemu nyingine tofauti na eneo ambalo tukio hilo la mauti yamemkuta.